Wang Yi asema China na Russia zimeanzisha uhusiano mpya wa kuigwa kati ya nchi kubwa
2024-03-07 11:26:29| cri

Kwenye mkutano na waandishi wa habari wa mkutano wa pili wa Bunge la 14 la Umma la China, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema China na Russia zimeanzisha uhusiano mpya wa kuigwa kati ya nchi kubwa ambao ni tofauti na ule wa wakati wa Vita Baridi.

Amesema nchi hizo mbili zitadumisha mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, ili kulinda usalama na utulivu wa kikanda na kimataifa.