China yatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kuwasiliana na kundi la Taliban la Afghanistan
2024-03-07 10:23:01| CRI

Naibu mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Geng Shuang alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kuwasiliana na kundi la Taliban la Afghanistan.

Amesema tangu kundi la Taliban lichukue madaraka mwezi Agosti mwaka 2021, hali ya ndani nchini Afghanistan imekuwa na utulivu kwa ujumla, huku uchumi na maisha ya watu yakiboreshwa pamoja na kupanuka kwa ushirikiano wa kikanda. Maendeleo haya mazuri yanastahili kutambuliwa. Hata hivyo amebainisha kuwa wakati huo huo, Afghanistan bado inakabiliwa na changamoto kubwa katika masuala ya hali ya kibinadamu, maendeleo ya kiuchumi, na tisho la ugaidi.

Bw. Geng Shuang alitoa taarifa katika baraza la usalama kwamba baraza hilo linapaswa kuelewa kwa upana zaidi kuhusu hali ya Afghanistan, kupanga suluhu kwa njia ya kimantiki zaidi kulingana na hali halisi ili kubeba jukumu muhimu na la kiujenzi katika kuleta maendeleo thabiti ya Afghanistan na kushirikishwa kwenye jumuiya ya kimataifa.