Msomi wa Nigeria: China ni mwenzi asiye na mbadala kwa maendeleo ya Afrika
2024-03-07 10:49:42| CRI

Karibu tena msikilizaji katika kipindi hiki cha Daraja kinachokujia kila siku za Jumapili muda kama huu kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Katika kipindi cha leo, tutakuwa na ripoti inayohusu msomi wa Nigeria ambaye ni mtafiti wa Taasisi ya Amani na Utatuzi wa Migogoro ya Nigeria Dkt. Olalekan Babatunde anayeipongeza China kwa kuwa mwenzi asiye na mbadala kwa maendeleo ya Afrika. Pia tutakuwa na mahojiano kutoka kwa Tom Wanjala wa CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi anayezungumza na mwanzilishi wa mchezo wa Kungfu Wu Shu ambao unashika kasi nchini Kenya.