CGTN Kiswahili yafanya mazungumzo kuhusu “Jinsi nchi za Afrika zinavyonufaika na fursa mpya za maendeleo ya kiuchumi ya China”mjini Nairobi
2024-03-07 10:49:28| CRI

Idhaa ya Kiswahili ya televisheni ya CGTN (CGTN Kiswahili) huko Nairobi imefanya mazungumzo kuhusu “Jinsi nchi za Afrika zinavyonufaika na fursa mpya za maendeleo ya kiuchumi ya China” yakihudhuriwa na watu zaidi ya 20 wakiwemo wakuu wa vyombo vikuu vya habari vya Kenya, wataalamu, wasomi na wafanyabiashara.

Washiriki wa mazungumzo hayo wamefanya mjadala wa kina kuhusu mada mbalimbali ikiwemo ripoti ya kazi ya serikali ya China, mafanikio yaliyopatikana na utawala wa China, njia ya China kuelekea kuwa ya kisasa na maendeleo yenye ubora wa juu yanavyotoa fursa kwa Afrika, China na Afrika kufanya ushirikiano wa pande mbalimbali na kukabiliana na changamoto za pamoja, China kuhimiza mfumo wa pande nyingi na utandawazi, huku wakikubaliana kuwa na imani thabiti kuhusu uhai na ustahimilivu wa China ukileta manufaa mengi zaidi kwa Afrika.

Vyombo vingi vya habari vya Afrika Mashariki ikiwemo KBC, KTN, KUTV vimeripoti kuhusu mazungumzo hayo.