Mauzo ya Rwanda kwa China yaongezeka kwa zaidi ya 80% katika 2023
2024-03-07 14:59:17| cri

Balozi wa China nchini Rwanda Bw. Wang Xuekun amesema mauzo ya Rwanda kwa China katika mwaka 2023 yaliongezeka kwa zaidi ya asilimia 87 na kuweka rekodi ya juu ya dola za kimarekani milioni 131. Ongezeko hilo linatokana na uuzaji wa kahawa, chai na pilipili kavu.