Wataalam wakutana nchini Kenya ili kuharakisha maendeleo ya utafiti katika Afrika Mashariki
2024-03-07 10:50:13| CRI

Wataalam wamekutana jana huko Nairobi, Kenya kuharakisha maendeleo ya utafiti katika Afrika Mashariki.

Kikao hicho cha tatu cha sayansi, teknolojia na uvumbuzi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kimehudhuriwa na wadau zaidi ya 300 wakiwemo maofisa waandamizi wa serikali, watafiti na wajumbe wa taasisi barani Afrika, wakipeana uzoefu, mbinu bora na matumizi ya teknolojia na utoaji wa uvumbuzi.

Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi ya Kenya Bw. Walter Oyawa amesema, kanda hiyo inataka kuweka kipaumbele katika utafiti wa kuendeleza bidhaa zitakazoongeza ubora wa maisha ya watu katika kanda hiyo, akiongeza kuwa kuna mahitaji ya dharura kufuatilia utafiti na uvumbuzi kwa sababu huu ni uti wa mgongo wa maendeleo ya jamii yoyote.