Waziri wa Mambo ya Nje wa China asema China itakuwa nguvu thabiti ya amani, utulivu na maendeleo ya dunia
2024-03-07 11:24:33| cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi leo amefanya mkutano na wanahabari kando ya mkutano wa pili wa Bunge la 14 la Umma la China.

Bw. Wang amesema kwa sasa mazingira ya dunia yanashuhudia mabadiliko makubwa, na jamii ya binadamu inakumbwa na changamoto nyingi. Ikikabiliwa na mazingira magumu na tete ya kimataifa, China itakuwa nguvu thabiti ya amani, utulivu na maendeleo ya dunia. Kwenye ripoti ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China, rais Xi Jinping alisema zama hii ni zama yenye changamato na pia yenye fursa. China itasimama kwenye mstari sahihi wa historia na maendeleo ya ustaarabu wa binadamu, kunyanyua bendera ya amani, maendeleo, ushirikiano na kunufaishana, kujitafutia maendeleo chini ya msingi wa kulinda kithabiti amani na maendeleo ya dunia, na kulinda vizuri zaidi amani na maendeleo ya dunia huku ukitafuta maendeleo yake yenyewe. Ripoti hiyo ilisisitiza kuwa Chama cha Kikomunisti cha China kinaboresha maisha ya wananchi wa China na kurejesha ustawi wa taifa la China, pia kinadhamiria kutafuta maendeleo ya binadamu na umoja wa dunia. Hayo ndiyo majukumu na wajibu wa China, na pia ni ndoto na malengo ya China.