Kenya yapokea wahamiaji wa nchi za nje zaidi ya milioni 1
2024-03-08 08:45:48| CRI

Ripoti kutoka Shirika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM) ilisema kuwa Kenya imewapokea wahamiaji wa kigeni zaidi ya milioni 1.05.

Mkuu wa ujumbe wa Kenya katika shirika hilo Bibi Sharon Dimanche jana alisema katika kongamano la wanawake huko Nairobi kwamba wahamiaji hao wa kimataifa ni pamoja na wakimbizi na wahamiaji wengine wanaotafuta usalama na fursa nchini humo. Wengi wa wahamiaji wa kigeni wanatoka nchi jirani za Kenya.

Alisema kuwa Somalia ndio nchi yenye idadi kubwa ya wahamiaji nchini Kenya, ikifuatiwa na Uganda, Sudan Kusini, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Afisa huyo ameongeza kuwa mojawapo ya sababu za wahamiaji wa kimataifa wanaoingia Kenya ni ukosefu wa utulivu wa kisiasa na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi katika nchi zao.