Zambia kuanza kukata umeme kwa saa 8 kila siku kutokana na ukame
2024-03-08 08:32:38| CRI

Shirika la Umeme la Zambia “Zesco Limited” limetangaza kwamba litaanza kukata umeme kwa saa nane kila siku kutokana na kiwango kidogo cha maji kinachosababishwa na ukame.

Shirika hilo limesema litatangaza mpango wa ratiba yake ya ukataji umeme kuanzia Jumatatu ikiwa ni moja ya hatua za kukabiliana na ukosefu wa umeme. Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Voctor Mapani amewaambia wanahabari kwamba uamuzi huu umetolewa baada ya kufikiria kwa makini hali iliyopo ya nishati ya taifa ambayo inaonesha ukosefu mkubwa wa umeme kutokana na kiwango kidogo cha maji.

Akitambua athari mbaya za maamuzi hayo kwa wateja, Mapani amesema shirika lake la umeme limedhamiria kufanya kila liwezalo kushughulikia changamoto hiyo na kurejesha usambazaji wa kawaida wa umeme haraka iwezekanavyo.