Rais Xi Jinping asisitiza kuendeleza mageuzi ili kuimarisha uwezo wa kimkakati kwenye maeneo yanayoibuka
2024-03-08 08:45:51| CRI

Rais Xi Jinping jana Alhamisi amelitaka jeshi la China liwe na moyo thabiti wa kubeba jukumu, kuendeleza mageuzi na kuhimiza uvumbuzi, ili kuimarisha kwa pande zote uwezo wa kimkakati kwenye maeneo yanayoibuka.

Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China na mwenyekiti wa kamisheni kuu ya jeshi, alitoa kauli hiyo wakati akihudhuria mkutano wa ujumbe wa Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China (PLA) na Kikosi cha Askari Polisi cha Watu wa China (PAP) kwenye kikao cha pili cha Bunge la 14 la Umma la China.

Rais Xi amesema uwezo wa kimkakati kwenye maeneo yanayoibuka ni sehemu muhimu ya mkakati wa kitaifa na uwezo wa kimkakati, na una umuhimu mkubwa katika kujenga nchi kubwa na kuendeleza ustawi mpya wa taifa kwa pande zote kupitia juhudi za kuijenga China kuwa ya kisasa.