Kinachoitwa utumikishwaji wa nguvu mkoani Xinjiang kimetajwa na wajumbe kutoka Xinjiang kuwa ni upuuzi
2024-03-08 15:02:14| cri

Wajumbe kutoka mkoa wa Xinjiang wanaohudhuria mkutano wa pili wa bunge la umma la 14 la China wamepuuza kile kinachotajwa kuwa ni utumikishwaji wa nguvu mkoani humo.

Akijibu swali kutoka kwa wanahabari, ofisa kutoka kijiji cha Saymahalla cha eneo la Luntai mkoani humo Bw. Akram Memtimin, amesema tuhuma kuhusu utumikishwaji wa nguvu ni upuuzi na amesema yeye mwenyewe anaweza kutumia uzoefu wake kuelezea hilo.

Amesema anajua kuwa vyombo vya habari vya nje vimekuwa vikieneza uongo kuhusu “utumikishwaji wa nguvu” kwenye sekta ya pamba mkoani Xinjiang na Marekani imeweka vikwazo dhidi ya bidhaa za pamba za Xinjiang.

Ofisa mwingine Jin Zhizen amesema mwaka 2023 uzalishaji wa pamba mkoani Xinjiang ulizidi tani milioni 5, ukiwa ni asilimia zaidi ya 90 ya pamba yote iliyozalishwa nchini China, na matumizi ya mashine katika uvunaji yalichukua asilimia 85