Rais wa China atoa salamu za rambirambi kwa rais wa Tanzania kufuatia kifo cha rais wa zamani wa nchi hiyo Bw. Ali Hassan Mwinyi
2024-03-09 20:51:27| cri

Rais Xi Jinping wa China tarehe 7 kwa niaba ya serikali ya China na watu wake, alitoa salamu za rambirambi kwa rais wa Tanzania kufuatia kifo cha rais wa zamani wa nchi hiyo Bw. Ali Hassan Mwinyi, akitoa salamu za rambirambi za dhati kwa serikali ya Tanzania na watu wake, pamoja na familia ya hayati Bwana Mwinyi.Rais Xi alisema, Bwana Mwinyi alikuwa mwanasiasa na kiongozi mahiri, rafiki wa watu wa China, na alitoa mchango mkubwa kwenye kuhimiza uhusiano kati ya China na Tanzania. 

Amesema China inapenda kushirikiana na Tanzania, kupanua na kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta mbalimbali, na kusukuma mbele maendeleo ya ushirikiano huo wa kimkakati na wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.