Kikao cha Pili cha Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la China chafungwa leo
2024-03-10 10:20:12| CRI

Kikao cha Pili cha Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la China kimefungwa leo asubuhi katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing. Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Rais wa China, na Mwenyekiti wa Kamisheni Kuu ya Kijeshi ya Chama Xi Jinping pamoja na viongozi wengine wa Chama na serikali wamehudhuria ufungaji wa kikao hicho.