Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) Jumamosi lilitoa taarifa likisema, AU ina wasiwasi mkubwa juu ya matishio ya kiusalama kwa maendeleo ya Afrika, matishio ambayo ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi barani Afrika.
Taarifa hiyo imetolewa baada ya mkutano uliofanyika hivi karibuni, ambao ulijadili hali ya sasa ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inayokumbwa na mapambano.
Baraza hilo limesisitiza tena wasiwasi wake kuhusu mapambano yanayotokea sehemu tofauti za Afrika, na kusema mapambano hayo na hali isiyo na usalama vinazuia maendeleo ya kijamii na kiuchumi barani Afrika. Baraza hilo pia limesisitiza ahadi yake ya kutimiza Ajenda ya mwaka 2063 ya Afrika.