AU yalaani utekaji nyara mkubwa wa watoto wa shule na wanawake nchini Nigeria
2024-03-11 08:44:48| CRI

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amelaani utekaji nyara wa watoto wa shule na wanawake uliotokea kaskazini magharibi mwa Nigeria, na kutoa wito wa kuachiwa huru mara moja bila masharti.

Mamlaka nchini Nigeria zinasema watu wenye silaha waliwateka nyara wanafunzi wasiopungua 287 katika mji wa Kuriga siku ya Alhamisi iliyopita, na inasemekana huu ni utekaji nyara mkubwa zaidi kutokea kwenye shule moja katika miaka ya hivi karibuni.

Bw. Faki amesema tukio hilo ni ushahidi mpya wa kuwepo kwa tishio la ugaidi na ukosefu wa usalama nchini Nigeria na hata bara zima la Afrika.