Baraza la mashauriano ya kisiasa la China lakamilisha mkutano, na kuhimiza kuleta mambo ya kisasa
2024-03-11 08:44:00| CRI

Kamati ya taifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), imekamilisha mkutano wake wa kila mwaka, na kutoa wito kwa wajumbe wake kuchangia umoja mkubwa wa China na mshikamano na kuunganisha nguvu kwa ajili ya kuendeleza mambo ya kisasa kwa China.

Viongozi wa China Rais Xi Jinping, Waziri Mkuu Li Qiang, na viongozi wengine waandamizi ikiwa ni pamoja na Zhao Leji, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi, na Han Zheng walihudhuria mkutano wa kufungwa kwa mkutano wa pili wa Kamati ya 14 ya Taifa ya Baraza hilo kwenye jumba la mikutano ya umma mjini Beijing.

Mkutano huo uliongozwa na Wang Huning, mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa. Azimio kuhusu ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya Kamati ya taifa ya baraza hilo, azimio la ripoti ya jinsi mapendekezo kutoka kwa washauri wa kisiasa yalivyoshughulikiwa tangu mkutano wa mwaka uliopita, ripoti ya uchunguzi wa mapendekezo mapya, na azimio la kisiasa kwenye mkutano wa pili wa Kamati ya taifa ya 14 ya baraza hilo, ziliidhinishwa kwenye mkutano mkuu.