IMF yatoa dola milioni 120 kwa Uganda kushughulikia kudorora kwa uchumi kufuatia COVID-19, na mfumuko wa bei
2024-03-11 23:45:30| cri

Bodi ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) imeidhinisha utoaji wa dola milioni 120 kwa Uganda baada ya mapitio ya tano ya mpango wa Upanuzi wa Usaidizi wa Mikopo (ECF) utakaoiwezesha Uganda kupokea hadi dola bilioni 1 kutoka kwa wakopeshaji wa kimataifa.

Haya ni mapitio ya nne chini ya mpango wa ECF yaliyoanza mwaka 2021, na kufanya jumla ya msaada huo kwa sasa kufikia dola milioni 870, takriban miezi 8 baada ya malipo ya mwisho ya kiasi kama hicho mwezi Juni mwaka jana.

IMF imesema pesa hizo zimeisaidia Uganda kupata nafuu kutokana na kudorora kwa uchumi kulikotokana na madhara ya Covid-19 na kupunguza kasi ya mfumuko wa bei, lakini kuna hatari nyingi ambazo zinaweza kurudisha nyuma mafanikio hayo, na kutaka kuendelea kwa mageuzi.