Serikali ya Tanzania kuomba kibali UNESCO kujenga barabara za lami hifadhi ya Serengeti
2024-03-11 14:46:57| cri

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka za hifadhi za Taifa imeamua kuomba kibali cha kujenga barabara za lami kwenye hifadhi ya Serengeti ili kurekebisha miundo mbinu inayoharibiwa kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Tanzania.

Msemaji mkuu wa Serikali ya Tanzania Bw. Mobhare Matinyi amesema mamlaka ya hifadhi ya wanyamapori ya Tanzania (TANAPA) inaandaa andiko la kuomba kukarabati barabara hizo kwa kiwango cha zege na lami. Amesema sababu kuu za kuomba kibali kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) ni kwamba hifadhi za Taifa katika nchi mbalimbali duniani huwa zinapata hadhi maalum ya kuorodheshwa kwenye urithi wa dunia ambayo inasimamiwa na UNESCO.