Mlipuko wa ugonjwa wa uti wa mgongo waua watu 22 kaskazini mwa Nigeria
2024-03-12 08:49:50| CRI

Mamlaka za Afya zimeripoti Jumatatu kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Uti wa mgongo (CSM) katika jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Yobe umesababisha vifo vya takriban watu 22 tangu Disemba 2023.

Hayo yamesemwa na afisa wa uchunguzi wa magonjwa na utoaji taarifa Haruna Umar, alipokuwa akiongea na wanahabari huko Yobe mji mkuu wa jimbo la Damaturu, na kuongeza kuwa jumla ya wagonjwa 636 waliothibitishwa wamerekodiwa katika maeneo sita ya serikali za mitaa ya jimbo hilo katika mlipuko wa sasa

Afisa huyo alisema mgonjwa wa kwanza aliyeshukiwa kuwa na ugonjwa huo aliripotiwa mnamo Disemba 24, 2023, na kuthibitishwa mnamo Januari 26. Alisema takriban watu 564 wamepona na kuruhusiwa kutoka hospitalini, akibainisha kuwa wagonjwa waliobaki walikuwa wakifuatiliwa na kutibiwa katika vituo vya kutengwa katika jimbo hilo.

Umar aliongeza kuwa serikali ya jimbo la Yobe inachukua hatua madhubuti za kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.