Katibu mkuu wa UM atoa wito wa kusimamisha vita katika mwezi wa Ramadhani huko Gaza na Sudan
2024-03-12 08:48:19| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres Jumatatu alitoa wito wa kusimamisha vita katika mwezi wa Ramadhani huko Gaza na Sudan.

Amesema mwezi wa Ramadhani umeanza, kipindi ambacho Waislamu kote duniani wanatekeleza ibada muhimu na kueneza thamani ya amani, maafikiano na mshikamano. Hata hivyo amesema mauaji, mashambulizi ya mabomu na umwagaji damu bado vinaendelea huko Gaza. Ametoa wito wa kuheshimu moyo wa mwezi wa Ramadhani kupitia kunyamazisha silaha, na kuondoa vikwazo vyote, ili kuhakikisha msaada wa uokoaji wa maisha unafika mahali husika.

Guterres pia alitoa wito wa kusimamisha uhasama kwenye kipindi cha mwezi wa Ramadhani huko Sudan.