Huawei yatoa mafunzo ya ujuzi wa digitali kwa zaidi ya vijana 240 kaskazini mwa Uganda
2024-03-13 08:40:02| CRI

Kampuni ya teknolojia ya China Huawei imetoa mafunzo kwa vijana 241 katika wilaya ya Alebtong, kaskazini mwa Uganda, na kuwapa ujuzi mbalimbali wa dijitali.

Huawei ilisema katika taarifa yake iliyotolewa Jumatatu iliyopita kwamba vijana hao walihitimu Machi 7 baada ya mafunzo ya wiki tatu.

Denis Obua, afisa mwandamizi wa chama tawala cha National Resistance Movement, aliipongeza Huawei kwa kutekeleza mpango wa DigiTruck, unaoendana na mpango wa maendeleo wa nchi hiyo.

DigiTruck, lori lililobadilishwa kuwa darasa la kompyuta, husafiri kutoka mkoa mmoja hadi mwingine, ambapo wakufunzi hufundisha watu biashara ya mtandaoni na utafiti kuhusu mtandao wa internet. Ni sehemu ya mpango wa TECH4ALL wa Huawei wa kukuza digitali jumuishi na endelevu kote duniani.