Rais wa Angola kufanya ziara nchini China
2024-03-13 09:34:00| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Hua Chunying jana alitangaza kuwa, Rais Joao Lourenco wa Angola atafanya ziara ya kitaifa nchini China kuanzia tarehe 14 hadi 17 Machi.

Wakati wa ziara hiyo, wakuu wa nchi hizi mbili watafanya mazungumzo na kushiriki kwa pamoja kwenye hafla ya kusaini nyaraka za ushirikiano.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang, Spika wa Bunge la Umma la China Zhao Leji pia watakutana na rais Lourenco kwa nyakati tofauti.