Tanzania na Rwanda kuboresha ushirikiano Bandari ya Dar es Salaam
2024-03-13 23:42:20| cri

Tanzania na Rwanda zimekubaliana kuweka mazingira bora yatakayosaidia kuongeza ufanisi wa matumizi ya Bandari ya Dar es Salaam, ikiwa ni moja ya njia za kusaidia kukuza uchumi wa nchi hizo mbili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, January Makamba wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Kigali, nchini Rwanda akiandamana na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Dkt. Vincent Biruta.

Mbali na usafirishaji, Waziri Makamba na Waziri Biruta wamejadili masuala mengine ya kipaumbele kwa ushirikiano wa nchi hizo mbili, ikiwemo nishati, kilimo na teknolojia.