Afrika Kusini yatoa wito wa kuweka mazingira wezeshi kwa wajasiriamali barani humo
2024-03-14 10:31:11| cri

Afrika Kusini imewataka viongozi na watunga sera kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya ustawi wa wajasiriamali barani humo.

Makamu wa rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile ametoa wito huo katika Mkutano wa siku mbili wa wajasiriamali wa Afrika (GEC+Africa) unaofanyika mjini Cape Town, Afrika Kusini, unaotarajiwa kumalizika leo. Amesema Afrika ni bara lenye fursa nyingi ambazo bado hazijagunduliwa, na pia ni kituo cha uvumbuzi na ubunifu kinachosubiri kufufuliwa tena.

Mkutano huo ulioandaliwa na kitengo cha Maendeleo ya Wafanyabiashara Wadogo chini ya Idara ya Maendeleo ya Afrika Kusini, umehudhuriwa na zaidi ya wajumbe 1,500, wakiwemo wawakilishi wa makampuni madogo, ya ukubwa wa kati na makampuni makubwa, wawekezaji, wabunge na wawakilishi wa mashirika mbalimbali.