Mlipuko waua 7 na kujeruhi 27 kaskazini mwa China
2024-03-14 09:43:40| CRI

Ofisi ya mji ya usimamizi wa mambo ya dhrura leo imetangaza kuwa watu saba wamefariki na wengine 27 kujeruhiwa kwenye mlipuko uliotokea jana Jumatano katika Mkoa wa Hebei kaskazini mwa China.

Kwa mujibu wa ofisi hiyo ya mji huo mlipuko huo, unaoshukiwa kusababishwa na uvujaji wa gesi, ulitokea saa 1:54 asubuhi ya Jumatano katika duka la kitongoji cha Yanjiao katika mji wa Sanhe. Majeruhi wote wamekimbizwa hospitalini, na majeraha yao si ya kutishia maisha. Kati ya majeruhi wote, 14 wameruhusiwa kutoka hospitalini. Uchunguzi unaendelea.