Msomi wa Somalia: Ripoti ya kazi ya serikali yaonesha kuwa serikali ya China imekuwa ikitoa kipaumbele kwa wananchi
2024-03-14 08:21:44| CRI

“Mikutano Miwili” ya China iliyofanyika hivi karibuni mjini Beijing imefuatiliwa sana na jamii ya kimataifa. Ripoti ya kazi ya serikali ya China ya mwaka 2024 imeeleza kuwa, kazi kuu ya serikali kwa mwaka huu ni kulinda na kuboresha maisha ya watu, kuimarisha na kufanya uvumbuzi katika usimamizi wa mambo ya kijamii, kushikilia wazo la kutoa kipaumbele kwa wananchi, kukuza utajiri wa pamoja, kuhimiza masikilizano na utulivu wa jamii, na kuzidi kuongeza neema, faida na usalama wa wananchi.

Akizungumzia suala hili, msomi wa Somalia Abdilahi Ismail Abdilahi amesema, ripoti hiyo imeonesha kuwa, serikali ya China inaendelea kulinda na kuboresha mahitaji ya kimwili na kiroho ya wananchi, pia inaonesha kuwa serikali ya China imekuwa ikitoa kipaumbele kwa wananchi.

Mbali na hayo, amesema mambo atakayoyakumbuka zaidi katika ripoti hiyo ni kuimarisha mawasiliano ya watu na utamaduni kati ya China na nchi za nje na kuongeza uwezo wa utangazaji duniani, kwani huo utakuwa msukumo kwa wageni wanaoishi nchini China kama yeye, na kuwahimiza watoe mchango mkubwa zaidi katika mawasiliano ya utamaduni kati ya China na nchi za nje.