Zaidi ya bunduki 6,000 zasalimishwa katika zoezi la msamaha wa kumiliki silaha nchini Zambia
2024-03-14 22:29:21| cri

Bunduki 6,500 zinazomilikiwa kinyume na sheria zimesalimisha na wananchi nchini Zambia tangu kutangazwa kwa zoezi la msamaha wa kumiliki silaha nchini humo mwaka 2011.

Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa nchi hiyo, Jack Mwiimbu amesema, bunduki hizo zilisalimishwa kwa lengo la kuziharibu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali za kuimarisha udhibiti wa silaha nchini humo. Amesema serikali ina wasiwasi na matukio ya hivi karibuni ya mashambulio ya silaha katika maeneo ya umma, na kuongeza kuwa mashambulio kama hayo hayataruhusiwa kuwa kitu cha kawaida.

Pia amesema, serikali imeanza kupitia rena sheria inayosimamia umiliki wa silaha ili kuweza kudhibiti hali hiyo.