Namibia yatarajia kukuza uchumi wake kutokana na kuongezeka kwa utafiti wa mafuta
2024-03-15 22:44:17| cri

Rais wa Namibia Nangolo Mbumba amesema, nchi hiyo inajiandaa kwa ukuaji wa uchumi wakati ikitarajia kutangaza makadirio halisi ya hifadhi ya mafuta baadaye mwaka huu kufuatia ongezeko la shughuli za utafiti zilizoanza mwaka jana, hususan katika maeneo ya bonde la Walvis na Orange.

Akizungumza wakati akihutubia taifa, rais Mbumba amesisitiza umuhimu wa maendeleo haya, akisema anatarajia kuwa maendeleo ya mafuta, gesi na utoaji wa hewa safi ya kijani yatasaidia kukua kwa uchumi wa nchi hiyo, ongezeko la ajira na ustawi.

Matumaini ya Namibia ni kuwa nchi inayozalisha mafuta yanaendelea kuongezeka, huku kampuni za kimataifa za mafuta zikiongeza juhudi za utafiti nchini humo.