Bei ya mafuta yashuka nchini Kenya
2024-03-15 10:45:17| cri

Mamlaka ya Kudhibiti Bei ya Kawi na Petroli nchini Kenya (EPRA) imetangaza kupunguzwa kwa bei za petroli, dizeli na mafuta taa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na EPRA, bei ya petroli ilishuka kwa Sh 7.21, dizeli Sh 5.09 huku mafuta taa yakishuka kwa Sh 4.49. Kutokana na hatua hiyo, katika jijini Nairobi, lita moja ya petroli itakuwa ikiuzwa kwa Sh 199.15, dizeli Sh 190.38 huku mafuta ya taa yakiuzwa kwa Sh 188.74.

Mamlaka hiyo imesema kuwa bei hizo mpya zimeanza kutekelezwa jana usiku na zitaendelea hadi Aprili 14, 2024.