Rais Xi Jinping wa China amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Angola Joao Lourenco, ambaye yuko mjini Beijing, China kwenye ziara ya kiserikali.
Akibainisha kuwa China na Angola kwa pamoja zilisherehekea miaka 40 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia mwaka jana, Rasi Xi amesema uhusiano kati ya nchi hizo mbili umepita changamoto za kimataifa na kufanikiwa kuwanufaisha watu wa nchi zao.
Amesema ushirikiano kati ya China na Angola ni ushirikiano wa Kusini-Kusini na ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea, ambazo pia ni marafiki wazuri.
Wakuu hao wawili wa nchi pia wametangaza kupandishwa kwa uhusiano wa nchi mbili kuwa ushirikiano wa kina wa kimkakati wa pande zote.