Baraza la Usalama laidhinisha mabadiliko ya kiufundi kwa UNMISS
2024-03-15 08:51:02| CRI

Baraza la Usalama limepitisha azimio la kuidhinisha mabadiliko ya kiufundi kwa mamlaka ya Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS).

Azimio nambari 2726 lililoungwa mkono kwa kauli moja na wanachama 15 wa baraza hilo, linaamua kuongeza muda wa UNMISS hadi Aprili 30, mwaka 2024, na kuidhinisha UNMISS kutumia njia zote zinazohitajika kutekeleza majukumu yake.

Marekebisho hayo ya kiufundi yataruhusu muda zaidi kwa wajumbe wa baraza kutathmini maandalizi ya uchaguzi wa Sudan Kusini na kujadili kuongezwa kwa mamlaka ya tume hiyo, ambayo ni pamoja na usaidizi wa kiufundi kwa uchaguzi wa Sudan Kusini.