UNHCR yasema mtoto mmoja mkimbizi kati ya wawili nchini Ethiopia ana utapiamlo
2024-03-15 08:52:17| CRI

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema mtoto mmoja mkimbizi kati ya wawili nchini Ethiopia wenye umri wa kati ya miezi 6 hadi miezi 59, ana utapiamlo.

Katika chapisho lake la hivi karibuni linaloitwa "Mapengo Muhimu katika Huduma za Lishe kwa Wakimbizi nchini Ethiopia" iliyotolewa Alhamisi, UNHCR ilifichua kwamba uchambuzi wa utafiti wake wa lishe uliofanyika katika kambi na maeneo 21 ya wakimbizi kote Ethiopia ulionesha kuwa watoto 95,334 kati ya 203,371, ikiwa ni asilimia 46.9, walionesha angalau aina moja ya utapiamlo, ambayo ni pamoja na kudumaa, uzito mdogo na upungufu wa virutubishi.

Lilisema licha ya mapungufu, akina mama hutoa lishe bora kwa watoto wachanga kuanzia chini ya umri miezi 6 kwa kuwezesha kuanza kunyonyesha mapema.

Kwa mujibu wa UNHCR, Ethiopia inahifadhi wakimbizi na wanaotafuta hifadhi zaidi ya 823,000, wengi wakitoka Sudan Kusini, Somalia na Eritrea, huku asilimia 47 ya wakimbizi wakiwa ni wanawake na wasichana, na asilimia 59 wakiwa ni watoto.