Madaktari wa Kenya wafanya mgomo kote nchini
2024-03-15 08:55:09| CRI

Madaktari wa Kenya Alhamisi walianzisha mgomo kote nchini, wakiishutumu serikali kwa kutoshughulikia malalamiko yao, ikiwa ni pamoja na kuinua nyadhifa na kutuma madaktari wanafunzi zaidi ya elfu nne.

Mgomo huo umedhoofisha huduma ya matibabu nchini humo, ambako wagonjwa hawawezi kuhudumiwa. Maeneo yanayoathiriwa na mgomo huo ni pamoja na Nakuru, Kwale, Kilifi, Migori na Mombasa.

Katibu mkuu wa Muungano wa madaktari na madaktari wa meno wa Kenya (KMPDU) Bw. Davji Atellah alisema wanafanya mgomo baada ya kushindwa kwa mazungumzo na serikali.