Utafiti uliofanywa na Mtandao wa Televisheni wa Kimataifa wa China (CGTN) na Chuo Kikuu cha Umma cha China kupitia Taasisi ya Uenezi wa Kimataifa ya Zama Mpya umeonyesha kuwa, vipimo vya demokrasia na mageuzi ya demokrasia vinavyotumiwa na Marekani kote duniani vinaleta misukosuko, migogoro na maafa zaidi duniani.
Kwa mujibu wa utafiti huo, watu waliohojiwa wamelalamikia vikali vitendo vya Marekani kukandamiza nchi nyingine, kujitafutia faida kibinafsi na kuongeza mifarakano kwa jamii ya kimataifa na mvutano wa makundi tofauti kwa kutumia suala la demokrasia.
Katika utafiti huo, asilimia 84.3 ya wahojiwa wanaona kuwa demokrasia tofauti inatakiwa kuwepo katika nchi zenye tamaduni tofauti, huku asilimia 84.8 ya wahojiwa wakiona kuwa nchi inatakiwa kuzingatia historia, utamaduni na hali ya kitaifa wakati inapochagua mfumo wa kisiasa.
Utafiti huo umefanyika baada ya kukusanya takiwmu kutoka kwa wahojiwa 39,315 kutoka nchi 32 duniani zikiwa ni pamoja na nchi zilizoendelea kama vile Marekani, Uingereza, Ujerumani, Canada, Uhispania, na Japan, pamoja na wale wanaotoka nchi zinazoendelea kama Brazil, Argentina, Afrika Kusini, Malaysia, Peru, na Pakistan.