Askari 8 wa ulinzi wa amani wajeruhiwa katika shambulio mashariki mwa DRC
2024-03-18 08:37:33| CRI

Askari wanane wa ulinzi wa amani wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamejeruhiwa katika shambulio lililotokea jumamosi iliyopita mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Tume hiyo imesema, shambulio hilo lilitokea Sake, mji ulio umbali wa kilomita 20 kutoka mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC.

Mkuu wa Tume hiyo Bintou Keita amelaani vikali shambulio hilo, na kusema mmoja kati ya majeruhi hali yake ni mbaya. Ametoa wito wa kusitisha mara moja mapigano kati ya makundi yote yenye silaha dhidi ya raia, na kurejea tena ahadi ya Tume hiyo ya kuimarisha doria za pamoja kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi vya DRC ili kulinda raia.