Mfalme Letsie III wa Lesotho amesema, katika miaka 30 iliyopita, nchi yake na China zimedumisha uhusiano mzuri, na anatarajia kuwa uhusiano huo utaendelea kuimarika na kuwa imara zaidi kadri muda unavyokwenda.
Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua yaliyofanyika katika makazi yake mjini Maseru, Mfalme Letsie amesema huu ni mwaka wa 30 tangu kurejeshwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Lesotho na China, na chini ya uhusiano huo, Lesotho imefaidika sana na msaada kutoka China.
Mfalme Letsie III amesifu mapendekezo ya China ikiwemo Pendekezo la Kusaidia Mageuzi ya Kiviwanda barani Afrika, Mpango wa China wa Kuunga Mkono Maendeleo ya Kilimo cha Kisasa barani Afrika na Mpango wa Ushirikiano wa China na Afrika katika Kuendeleza Vipaji.