Serikali ya Tanzania yaanzisha mageuzi ya kimahakama, kijamii na kiuchumi
2024-03-18 14:09:01| cri

Ikiwa ni jitihada za kuimarisha upatikanaji wa haki kwa raia wake, serikali ya Tanzania imeanza kuchukua hatua za kuleta mageuzi, kwa kujenga mahakama zaidi kote nchini Tanzania. Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba Dk Pindi Chana, amezindua miradi mingi yenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa miundombinu ya utoaji haki nchini Tanzania.

Ujenzi wa mahakama hizi umetajwa kuwa ni sehemu ya dhamira ya serikali ya kujenga uaminifu miongoni mwa raia katika mfumo wa mahakama. Dk Chana ameangazia kuanzishwa kwa 'Mahakama inayohama' kama mpango muhimu wa kushughulikia malalamiko katika maeneo yenye watu wengi na maeneo ya migogoro. Juhudi hizo zimeleta matokeo ya kuridhisha, huku mrundikano wa kesi ukipungua kwa kiasi kikubwa hadi asilimia 4 tu, na hivyo kuashiria kuimarishwa kwa ufanisi wa mahakama.