Waziri mkuu wa Israel asema jeshi la Isarel litafanya operesheni ya ardhini huko Rafah kama lilivyopangwa
2024-03-18 14:15:49| cri

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema jeshi la Isarel litafanya opresheni ya ardhini kama lilivyopangwa huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Bw. Netanyahu aliposhiriki kwenye mkutano wa baraza la mawaziri tarehe 17, alisema hakuna shinikizo lolote la kimataifa linaloweza kuzuia Isarel kutimiza malengo yake yote ya operesheni za kijeshi katika Ukanda wa Gaza, ikiwa ni pamoja na kuangamiza kundi la Hamas, kunusuru mateka wote wanaoshikiliwa, na kuhakikisha Ukanda wa Gaza hautaleta tishio tena kwa Israel. Ili kutimiza malengo hayo, jeshi la Israel litafanya operesheni ya ardhini huko Rafah kama lilivyopangwa.