Xi ampongeza Putin kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Russia
2024-03-18 18:17:13| cri

Rais wa China Xi Jinping leo amempongeza Vladimir Putin kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Russia.

Xi amesema katika miaka ya hivi karibuni, watu wa Russia wameungana pamoja, kushinda changamoto na kupiga hatua thabiti kuelekea maendeleo na ustawi wa taifa, akiongeza kuwa kuchaguliwa tena kwa Putin kama rais wa Russia kunaonyesha kikamilifu uungaji mkono wa watu wa Russia kwake.

Amesema Russia hakika itapata mafanikio makubwa zaidi katika maendeleo ya kitaifa na ujenzi chini ya uongozi wa Putin.