Putin ashinda uchaguzi wa rais wa Russia
2024-03-18 08:34:36| cri

Matokeo yaliyotangazwa na Tume Kuu ya Uchaguzi ya Russia mapema leo yameonyesha kuwa, rais wa sasa wa nchi hiyo, Vladmir Putin, anaongoza wagombea wengine kwa tofauti kubwa ya asilimia 87.19% ya kura, na ameshinda uchaguzi wa rais.

Kwenye hotuba yake aliyoitoa leo asubuhi katika makao makuu ya kampeni, Bw. Putin amewashukuru wapiga kura wote kwa kumuunga mkono, akisema Russia ni familia kubwa, na matokeo ya uchaguzi huo yanaonyesha imani na matarajio ya wapiga kura, kazi zote za nchi zitakamilika, na Russia itasonga mbele na kuwa imara zaidi na yenye ufanisi zaidi.

Uchaguzi wa rais ulifanyika nchini Russia kuanzia tarehe 15 hadi 17 mwezi huu, na kulingana na sheria za uchaguzi wa rais, mtu anayepata zaidi ya asilimia 50 ya kura katika uchaguzi atachaguliwa kuwa rais.