Sudan Kusini yafunga shule kutokana na joto kali
2024-03-18 23:06:27| cri

Sudan Kusini imetangaza kufungwa kwa shule zote kwa muda usiojulikana kutokana na joto kali katika siku chache zilizopita.

Waziri wa Afya wa Sudan Kusini Bibi Yolanda Awel Deng, amesema sehemu nyingi za Sudan Kusini zinakabiliwa na wimbi la joto linalotarajiwa kudumu kwa wiki mbili zenye hali joto kati ya nyuzi joto 41 na nyuzi joto 45 sentrigredi. Bibi Yolanda amesema serikali imeamua kuchukua hatua mbili, moja ni kufunga shule zote kuanzia Machi 18, na mbili, wakati wa kufungwa kwa shule hizo wazazi wanashauriwa kuwazuia watoto wao kucheza nje kwa muda mrefu na pia wawafuatilie watoto, hasa vijana, kuangalia dalili za uchovu unaotokana na joto na kiharusi.