Maonesho makubwa ya nishati ya jua yafunguliwa nchini Afrika Kusini
2024-03-19 08:31:31| cri



Maonesho makubwa ya nishati endelevu barani Afrika, nishati ya jua na uhifadhi Afrika 2024, yamefunguliwa jana huko Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Kampuni ya Terrapinn imesema, maonesho hayo ya siku tatu yanashirikisha zaidi ya waoneshaji 350 wa ndani na nje ya Afrika Kusini.

Ofisa wa kampuni ya Terrapinn Bw. Gina Bester amesema, ni muhimu sana kwa nishati na sekta ya nishati ya jua kuungana na kuelekea kwa pamoja katika mustakabali endelevu zaidi, huku ikitafuta utafiti wa suluhisho lenye uvumbuzi.