Wizara ya kilimo ya Tanzania kuzindua benki ya mbegu
2024-03-19 10:32:15| cri

Katibu Mkuu wa wizara ya Kilimo ya Tanzania Bw. Gerald Mweli anatarajiwa kuzindua benki ya kisasa ya mbegu yenye uwezo wa kuhifadhi mbegu kwa miaka 100 inayomilikiwa na Taasisi ya Utafiti na Uendelezaji wa Mazao ya Mbogamboga Duniani (WVC).

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dk Gabriel Rugalema amesema benki hiyo kubwa ya kisasa Afrika, inaweza kuinua uchumi kwani ndio malengo yaliyokusudiwa na katika kukuza kilimo cha mboga mboga Tanzania na Afrika. Amesema karne ya kizazi kijacho inaweza kupata na kusikia historia ya mbegu mbalimbali kama vile mchicha lishe kutokana na benki hiyo kuwa na vifaa vya kisasa vya kuhifadhi mbegu kwa muda huo.