Rais wa China apongeza Bw. Vladmir Putin kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Russia
2024-03-19 08:31:44| cri

Rais Xi Jinping wa China jana alimpigia simu Bw. Vladmir Putin kumpongeza kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Russia.

Rais Xi amesema, katika miaka ya hivi karibuni, watu wa Russia wameshikamana ili kukabiliana na changamoto na kusonga mbele kithabiti katika barabara ya maendeleo na ufufuaji wa taifa.

Amesema anaamini kuwa chini ya uongozi wa Bw. Putin, Russia inaweza kufikia mafanikio makubwa katika maendeleo ya kitaifa na ujenzi.

Rais Xi amesema, China inatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na inapenda kudumisha mawasiliano ya karibu na Russia ili kukuza maendeleo endelevu ya ushirikiano wa kimkakati wa pande zote katika enzi mpya kati ya China na Russia na kunufanisha nchi na watu wake.