Rais wa China afanya ziara ya ukaguzi mkoani Hunan
2024-03-19 20:39:29| CRI

Rais Xi Jinping wa China amefanya ziara ya ukaguzi mjini Changde, mkoani Hunan, ambapo alitembelea Mtaa wa Mto, Kijiji cha Gangzhongping, tarafa ya Xiejiapu katika Mtaa wa Dingcheng.

Katika maeneo hayo, rais Xi alifahamishwa kuhusu ukarabati wa mtaa wa kitamaduni na kihistoria, usimamizi wa mazingira ya maji mjini, kilimo cha majira ya mchipuko, na ufanisi wa usimamizi wa ngazi ya shina.

Alipotembelea eneo la vielelezo la uzalishaji wa nafaka kwenye tarafa ya Xiejiapu, rais Xi aliwasiliana na wakulima, wataalamu wa kilimo, makada wa shina na wanakijiji ili kufahamu zaidi maendeleo ya maandalizi ya kilimo cha majira ya mchipuko.