FAO: Baa la njaa laweza kutokea wakati wowote huko kaskazini mwa Gaza
2024-03-19 23:20:45| cri

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetoa ripoti kuhusu usalama wa chakula likitahadharisha kuwa janga la njaa linaweza kutokea wakati wowote katika eneo la kaskazini mwa Ukanda wa Gaza. Pia imesema kutokana na kutositishwa kwa vitendo vya uhasama na msaada wa kibinadamu kuendelea kutopatikana, maeneo mengine ya Ukanda huo pia yatakabiliwa na hatari ya baa la njaa katika siku zijazo. Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Beth Bechdol amesema hali ya ukosefu wa usalama wa chakula katika Ukanda wa Gaza imekuwa mbaya zaidi kuwahi kurekodiwa.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alipozungumzia ripoti hiyo alisema janga la kibinadamu lililotokea huko Gaza limesababishwa na binadamu, akitoa wito kwa Israel kuhakikisha "upatikanaji kamili na usio na kikomo" wa misaada ya kibinadamu katika Ukanda huo.