Shule ya sekondari ya Uganda yashinda tuzo ya kikanda ya uvumbuzi wa kilimo
2024-03-19 10:26:46| cri

Timu ya wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Rise and Shine iliyopo mjini Kampala imepata ushindi wa tuzo ya uvumbuzi wa kilimo baada ya kuvishinda vikundi vingine 12 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Jopo la majaji lilistaajabishwa na umahiri wa vijana hao katika harakati zake na maonesho ya uvumbuzi unaoweza kutekelezeka zaidi. Taarifa iliyotolewa baada ya mashindano hayo imesema katika maonesho ya ubunifu, Timu ya Imperial Tech kutoka Shule ya Sekondari ya Rise and Shine huko Ntinda, Uganda, imeibuka kuwa mabingwa wa mwaka huu.

Mashindano hayo yalianzishwa ili kuwapa washiriki nafasi ya kujifunza darasani, na kuwapa ujuzi wa kivitendo unaohitajika ili kuleta masuluhisho ya kibunifu kwa matatizo ya dunia halisi.