Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema, ukosefu wa usalama katika kanda ya Afrika Mashariki huenda ukaendelea mpaka katika robo ya pili ya mwaka huu.
Ripoti iliyotolewa na Shirika hilo imesema, hali hiyo inatokana na mapigano, kupanda kwa gharama za maisha, na mlipuko wa magonjwa. WFP pia imesema, changamoto zinazotokana na mapigano zinaweza kudhibitiwa na msimu wa mvua kubwa kuliko kawaida ambao utatoa fursa kwa eneo hilo kuendelea kufufuka kutoka kwenye msimu wa ukame ulioanza mwaka 2020 hadi mwaka jana.
Mpaka kufikia mwezi Machi, eneo la Afrika Mashariki lilikadiriwa kuwa na watu milioni 54 wanaokabiliwa na ukosefu wa chakula, huku Sudan, Ethiopia na Sudan Kusini zikiwa na hali mbaya zaidi.