WMO latoa tahadhari nyekundu baada ya viwango vingi vya mabadiliko ya tabianchi kuweka rekodi mpya
2024-03-20 10:57:45| cri

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) imeonyesha kuwa mwaka 2023 viwango vingi vya mabadiliko ya tabianchi viliweka rekodi mpya , ikiwemo mkusanyiko wa gesi chafu, halijoto ya uso wa ardhi, joto na tindikali baharini, kupanda kwa usawa cha bahari, na uyeyukaji wa barafu n.k. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mwaka 2023 ulikuwa mwaka mwenye joto kali zaidi kuwahi kurekodiwa, halijoto ya uso wa ardhi imeongezeka kwa nyuzi joto 1.5 sentigredi ikilinganishwa na nyakati kabla ya viwanda.

Pia ripoti hiyo imeeleza kuwa majanga yanayosababishwa na joto kali, mafuriko, ukame, moto wa misituni na vimbunga vya kitropiki yameleta taabu kwa maisha mamilioni ya watu na kusababisha hasara ya kiuchumi ya mabilioni ya dola za kimarekani.