Baadhi ya maeneo ya Rwanda yakabiliwa na joto la juu ya wastani
2024-03-20 22:56:24| cri

Shirika la hali ya hewa la Rwanda limesema maeneo mbalimbali ya Rwanda yamekabiliwa na joto la juu kwa wastani wa nyuzi joto 20 hadi nyuzi 30, ambalo limezidi kidogo kiwango cha juu cha wastani cha joto cha muda mrefu, ikilinganishwa na kipindi kama hicho hapo awali.

Maeneo mengi ya mji wa Kigali, Wilaya za Bugesera na Nyagatare, eneo la Amayaga, bonde la Bugarama, na baadhi ya maeneo ya wilaya za Ngoma na Gatsibo yanakabiliwa na halijoto ya juu zaidi kati ya nyuzi 28 na nyuzi 30 sentigredi.

Shirika la hali ya hewa limesema kupungua kwa kiasi cha mvua na siku za mvua kulitarajiwa kwa siku 10 kuanzia Machi 11 hadi Machi 20.